Story by Our Correspondents-
Waziri wa elimu nchini Prof Goerge Magoha ametoa tarehe mpya ya kufungwa kwa shule zote nchini ili kupeana nafasi ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Waziri Magoha amesema shule hizo zitafungwa rasmi kuanzia tarehe mbili mwezi huu yani siku ya Jumanne hadi tarehe 11 siku ya Alhamis ambapo shule hizo zitafunguliwa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ili kuendelea na ratiba ya masomo.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Waziri Magoha amesema uamuzi huo umechuliwa baada ya mashauriano na wadau wa sekta ya elimu ili kuruhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao umeratibiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 9.
Iwapo mshindi hatopatikana katika duru ya kwanza ya uchaguzi ama mkenya yeyote kuwasilisha kesi Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais basi tarehe hizo za kufunguliwa kwa shule huenda zikabadilika na hatua hiyo huenda ikaathiri mitihani ya kitaifa iliyopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.