Wakaazi katika eneo la Maweni huko Nyali kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti hiyo kukarabati mitaro ya kupitisha maji taka katika eneo hilo ili kuepuka mafuriko msimu huu wa mvua.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa kituo cha afya cha Maweni Peter Otieno wakaazi hao wamedai kuwa kwa takriban juma moja sasa shughuli za kawaida zimetatizika eneo hilo kutokana na mafuriko yanayokumba maeneo yao.
Akiongea na mwanahabari wetu Peter amesema kuwa kuna hatari ya wakaazi kukumbwa na mkurupuko wa maradhi kutokana na maji taka yanayojaa eneo hilo.
Kwa upande wake Policarp Otieno mmoja wa wakaazi eneo hilo ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuwajibikia tatizo hilo.
Taarifa na Sammy Kamande.