Picha Kwa Hisani.
Baada ya kundi la muziki wa Genge ‘The Kansol’ kusambaratika, wanamuziki Mejja na Madraxx waliendelea kurekodi muziki kila mmoja kivyake, huku Kid Kora akikaa kimya na kupotea kwenye sanaa ya muziki.
Kabla ya wanamuziki hao kutengana, The Kansol walivuma kwa nyimbo kama vile; Bablas, Tunakubali, Nyongwa, Double tap miongoni mwa zingine nyingi.
Madraxx sasa amejitokeza na kuzungumzia swala hilo na kufichua kwamba hakuna chuki kati yao.
Aidha, Madraxx alisema kuwa alipoona taarifa za kundi hilo kusambaratika, alijaribu kumpigia simu Kid Kora, ambaye alimrushia maneno makali.