Mtangazaji Aisha Abushiri maarufu kama Mamaa Madikodiko ndiye atakayeongoza kipindi cha Mirindimo Ya Kimwambao.
Madikodiko anachukua usukani wa kipindi hicho kutoka kwa Mimu Mohammed ambaye kwa sasa anarudi katika kitengo cha uhariri wa habari.
“Ni fursa adimu kuweza kupata nafurahia kupata fursa hii na Inshallah nipo na matumaini kuwa mambo yatakuwa bora zaidi kwangu na kwa kituo ninachokitumikia kwa sasa,”amesema Madikodiko.
Kando na utangazaji Madikodiko ni mama, muigizaji na mfanya biashara.