Mamaa Madikodiko amefichua makuu aliyoyapitia wakati alipoachishwa kazi ghafla.
Madikodiko ambaye kwa sasa amechukua usukani wa kipindi cha Mirindimo Ya Kimwambao katika stesheni ya Radio Kaya amesema kuwa alipitia kipindi kigumu ikizingatiwa kuwa mamake mzazi ni anaugua saratani.
Mtangazaji huyo amesema kuwa katika kipindi hicho alijihisi mpweke kwani wengi wa wale aliowadhania kuwa ni marafiki hawakuitika mwito wake pale alipohitaji msaada kutoka kwao.
“Kufutwa kwangu kazi kulijiri ghafla, sio jambo ambalo mtu ulikuwa unaweza kujipanga. Ni katika kipindi hichi ambapo nilijifunza mengi lakini kubwa zaidi niliwajua marafiki wa kweli. Wapo watu ambao wahakunishika simu zangu pale nilihitaji msaada,ni kitu kilichonivunja moyo na kunitamausha lakini ndivyo walivyo binadamu,” amesema Madikodiko.
Kando na hayo mtangazaji huyo amewashauri watangazaji wenzake kutomuamini mtu yoyote maishani na kujieka tayari kwa jambo lolote.
“Iwapo upo katika tasnia hii ya utangazaji na upo na nafasi nzuri, jitengenezee maisha. Jipange na mapema ndio usijipate pabaya,” amesema Madikodiko.
Msikilize Mamaa Madikodiko kila siku ya juma kuanzia saa saba na robo mchana kwenye Mirindimo Ya Kimwambao.
Pole nimitihan ya dunia Allah azidi kumwilika
Show iko poa naipata loud n clear nikiwa iraq, naomba mnichezee Sharo baro wa bamba by Ricky melodies
Hao ni wanadamu.Pia afadhali wasishike simu na pia wasikusaidie tu .La kusitisha zaidi watakusimanga
Dats how people are in tum of troubles they all run away.just like me I was in th same situation