Mwenyekiti wa shule za udereva ukanda wa Pwani John Magara ameitolea mwito wizara ya uchukuzi nchini kuibuka na mikakati maalum ya kuwaadhibu madereva wanaotumia dawa za kulevya wanapohudumu.
Akiongea mjini Mombasa Magara amedai kuwa madereva wengi hutumia aina tofauti za mihadarati wakiwa kazini akitaja pombe na bangi, hali ambayo imesababisha ongezeko la ajali barabarani.
Magara amewahimiza madereva kuwa makini barabarani wakati huu ambapo wanafunzi wamefungua shule kwa muhula wa tatu.
Amehimiza madereva kusomea ujuzi wa kuendesha magari katika shule za udereva ili kuwa na elimu ya kutosha kuhusu uendeshaji magari.
Taarifa na Hussein Mdune.