Story by Gabriel Mwaganjoni –
Madereva wa masafa marefu nchini wamezidi kulalamikia hali tata ya kiusalama inayowakumba hasa katika barabara kuu ya Mombasa -Nairobi na mataifa jirani kufuatia kukithiri kwa wizi katika barabara hizo.
Mwenyekiti wa muungano wa madereva wa masafa wa marefu nchini Roman Waema amesema hali hiyo ni ya kusikitisha huku akiitaka Serikali kuliangazia swala hilo.
Waema amesema licha ya kilio cha madereva hao kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, Serikali imewapuuzilia mbali na kuwawacha wakiendelea kuvamiwa, kuumizwa na wengine wao kuuwawa mikononi mwa wavamizi hao.
Waema amesema hali ni tata zaidi nchini Sudan Kusini licha ya Serikali hiyo kuwaahidi usalama wa kutosha madereva hao.
Tayari madereva hao wa masafa marefu wamesitisha safari zao za nchini Sudan kusini kufuatia msururu wa visa vya mauaji ya madereva kutoka nchini Kenya.