Kamanda wa trafiki eneo la Malindi George Naibei amewataka wahudumu wa bodaboda sawa na madereva wa uchukuzi wa umma katika eneo hilo kuzingatia sheria za trafiki wanapokua barabrani ili kuepuka ajali.
Akiongea na wanahabari mjini humo Naibei amesema kuwa hatua ya madereva kutofuata sheria imechangia pakubwa ajali za barabarani zinazoshuhudiwa katika eneo hilo.
Naibei aidha amesema kuwa idara ya trafiki eneo hilo inafuatilia kwa karibu utendakazi wa madereva wa eneo hilo, huku akisema kwamba watakopatikana wakikiuka sheria hizo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Kauli ya kamanda huyo inajiri huku visa vya ajali za barabrani vikionekana kuongezeka nchini.
Taarifa na Esther Mwagandi.