Joseph Mwarandu
Wazee wa Kaya huko Malindi kaunti ya Kilifi wamepongeza juhudi zinazoendelezwa na serikali kukabiliana na jinamizi la ufisadi nchini.
Katibu wa Muungano wa Utamaduni mjini Malindi MADCA, Joseph Mwarandu, amesema ufisadi ni janga lililokithiri nchini ambalo linapaswa kukomeshwa.
Mwarandu amesema kwamba serikali imeonyesha ari kukabiliana na janga hili akihimiza wakenya kuunga mkono juhudi hizi ili kukabiliana na ufisadi ambao umeendelea kuliathiri taifa.
Taarifa na Esther Mwagandi.