Story by Janet Shume-
Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu ametangaza rasmi uteuzi wa shule za upili kwa wanafunzi waliokamilisha mitihani ya KCPE mwaka 2022, kwamba watajiunga na shule za upili kuanzia tarehe 6 haid 15 mwezi Februari.
Akizungumza na Wanahabari jijini Nairobi, Machogu amesema wanafunzi zaidi ya milioni 1.2 wameteuliwa katika shule mbalimbali za upili kwa kuzingatia alama walizopata kwenye mtihani wa KCPE.
Machogu amesema jumla ya wanafunzi 38,972, wanafunzi wa Kike wakiwa 18,794 na wale wakiume wakiwa 20,198 wameteuliwa kujiunga na shule za upili za kitaifa huku wanafunzi 199,027 watajiunga na shule za kaunti na wanafunzi 228,160 wakijiunga na shule za Extra County.
Hata hivyo ameweka wazi kwamba kaunti za Nairobi, Kilifi, Mombasa, Kajiado, Turkana, Kwale, Garissa, Taita taveta, Kitui na Narok kama zinazoshuhudia uhab wa shule za Sekondari ikizingatiwa kwmaba idadi kubw aya wanafunzi wanaokamilisha darasa la nane kila mwaka.
Wakati uo huo amedokeza kwmaba serikali itaendelea kutekeleza jukumu lake la kumlipia kila mwanafunzi wa shule za upili shilingi 22,244 akisema hakuna mabadiliko yoyote ya karo yaliofanyika huku akiwataka wazazi kuondoa hofu ya kuongezeka kwa karo shuleni.
Akigusia kuhusu wanafunzi waliokamilisha mtihani wa darasa la sita wa KPSEA, Waziri Machogu amesema serikali inalenga kutumia shilingi bilioni 9.6 kusimamia elimu ya Junior Secondary ikiwa ni gredi ya saba, nane na tisa katika shule zote za umma kuanzia mwaka huu huku akitoa onyo kali kwa walimu wakuu watakaowahangaisha wazazi ili kutoa malipo ya ziada kinyume cha sheria kwamba watachukuliwa hatua.