Story by Our Corresponents-
Waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu amesema wanafunzi 252 wa mtihani wa KCPE kutoka vituo tisa vya kufanyia mitihani walinaswa wakishiriki udangayifu na kupewa alama sufuri katika somo hilo.
Machogu amesema asilimia 100 ya wanafunzi zaidi ya milioni 1.2 waliofanya mtihani huo wa KCPE watapata nafasi kujiunga na shule za upili huku akihiji kwamba wanafunzi 2,417 wenye uwezo maalum na wanafunzi 7 kati yao wamepata alama ya 400 na zaidi.
Akizungumza wakati wa halfa ya kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCPE katika jumba la mitihani house jijini Nairobi, Waziri Machogu amesema wanafunzi waliokamilisha gredi ya 6 wataendeleza masomo yao ya Junior secondary katika shule za msingi wanazosomea.
Vile vile ametangaza kwamba zoezi la kusajili wanafunzi waliokamilisha mtihani wa kitaifa wa KCPE katika shule mbalimbali za upili ikiwemo zile za kitaifa na kaunti litakamilika rasmi Januari 16 mwaka ujao huku mihula ya masomo ikirejea kama kawaida kuanzia Januari mwaka ujao.