Story by Our Correspondents-
Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu ameweka wazi kwamba serikali haina malengo ya kuongeza karo katika shule za umma jinsi baadhi ya watu wanavyodai nchini.
Waziri Machogu amesema karo ambayo wazazi watalipa kuanzia mwezi Januari mwaka ujao baada ya shule kufunguliwa rasmi Januari 23, sio nyongeza ya karo bali ni kutokana na kurejeshwa kwa hali ya kawaida ya kalenda ya masomo.
Akizungumza katika kaunti ya Wajir wakati wa ziara yake ya kielimu ya tathmini maandalizi ya mitihani ya kitaifa, Waziri Machogu amesema tangazo lililotolewa na Katibu katika Wizara ya elimu nchini Dkt Julius Jwan halihusiani na nyongeza ya karo.