Wakaazi wa eneo la Hindi Kaunti ya Lamu wamesisitiza kwamba uvamizi unaotekelezwa katika eneo hilo na visa vingi vya ukosefu wa usalama vimechangiwa na mabwenyenye wanaonyakua ardhi zao kila uchao.
Wakiongozwa na mkuu wa polisi jamii katika eneo hilo Peter Mwaura, Wakaazi hao wamesema kwamba uvamizi huo unalenga kuwatimua kwenye mashamba yao ili mabwenyenye hao wamiliki ardhi zao na kuwasaza maskwota.
Mwaura ameitaka Serikali kuwapimia Wakaazi hao ardhi zao ili migogoro hiyo na msukosuko wa kiusalama wa mara kwa mara katika eneo hilo ukomeshwe.
Kwa upande wake, Kiongozi mkuu wa mashtaka ya umma nchini anayekutana na Wakaazi wa Kaunti ya Lamu ili kusikiza lalama zao, amesema kwamba kwa kipindi cha juma zima la vikao vyake Kaunti ya Lamu amebaini swala la ardhi ni tata mno katika Kaunti hiyo na ni lazima litanzuliwe.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.