Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo ameamrisha Manaibu Kamishna wa magatauzi yote madogo ya kaunti ya Kwale pamoja na maafisa wa usalama kufanya msako na kuyafunga mabanda ya video yanayoendesha shughuli zake bila leseni.
Akiongea na Wanahabari, Ngumo amesema hatua hiyo itaimarisha zaidi usalama na nidhamu kwa vijana wadogo katika kaunti hiyo.
Ngumo amesema mabanda hayo yako karibu na shule na maakazi ya watu hali ambayo inachangia watoto kutazama filamu za ngono zinazowapotosha kimaadili.
Taarifa na Mariam Gao.