Kamati ya dharura ya kukabiliana na janga la Corona kaunti ya Kwale imewapa mamlaka zaidi mabalozi wa nyumba kumi ili kuhakikisha wanalinda mipaka ilioko katika maeneo yao.
Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema mabalozi wa nyumba kumi waliopewa jukumu hilo ni wale walioko katika maeneo ambayo hakuna maafisa wa polisi.
Ngumo amesema hatua hiyo itasaidia pakubwa kuhakikisha marufuku ya kuingia au kutoka katika kaunti hiyo inatekelezwa vilivyo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.
Kamishna huyo wa kaunti ya Kwale amedokeza kuwa wakaazi wengi wa kaunti hiyo bado hawajazingatia agizo la kuvaa barakoa wanapokua katika maeneo ya umma.