Mabaharia mjini mombasa wamejitokeza na kuitaka Serikali kufanya mabadiliko ya uongozi kwa mamlaka ya ubaharia nchini KMA Kwa kile wanachodai kuwa imezembea kwenye majukumu yake ya kutatua changamoto zinazowakumba mabaharia.
Wakiongozwa na Hassan Kombo Ismail wamesema kuwa visa vya unyanyasaji kwa mabaharia wa Kenya vimekithiri mno kwani wamesema mabaharia humu nchini hawathaminiwi kuliko wale wakigeni hatua anayoitaja kuvunja moyo za mabaharia.
Mabaharia hao aidha wameongezea kwamba licha ya wao kupeleka malalamishi yao kwa mamlaka hiyo hakuna hatua zozote zinachuliwa na kupelekea wengi wao kuishi bila ajira.
Taarifa na Hussein Mdune.