Story by Our Correspondents –
Kongamano la Maaskofu wa Kanisa katoliki nchini limemtaka Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Dkt William Ruto kusitisha malumbano yao ya kisiasa na kushirikiana kama viongozi wa taifa hili.
Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa jimbo kuu la Nyeri Anthony Muheria wamesema huu ni wakati mwafaka wa viongozi hao kuungana ili kusitisha joto la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa.
Askofu Muheria amesema kuungana kwa viongozi hao kutachangia taifa hili kuandaa uchaguzi huru, haki na amani sawia na kuzuia kushuhudiwa kwa mihemeko ya kisiasa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambaye pia na Askofu wa jimbo kuu la Mombasa Martin Kivuva amesema maaskofu hao wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa makanisani na kuwataka viongozi kuhudhuria ibada ya Misa sawa na waumini wengine.