Story by: Janet Shume.
Wakaazi wa eneo la malomani katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wameshuhudia kisa cha kushangaza hapo jana baada ya kushuhudia nyoka ambaye hata licha ya kukatwa mapanga na wakaazi ilichukua muda kuuwawa.
Sidi Ngema mmoja wa wakaazi walioshuhudia tukio hilo amesema baada ya nyoka huyo kuuliwa alipatikana amemeza mwiko wa kupikia, hali iliyowatamausha zaidi wakaazi.
Hata hivyo, kutokana na tukio hilo sasa wakaazi hao wamejawa na wasiwasi mkubwa wakilihusisha tukio hilo moja wapo wa visa vya mazingaombwe ama ushirikina unaoendelezwa eneo hilo.