Taarifa na Charo Banda.
Maafisa wa tume ya EACC tawi la Malindi wamewatia nguvuni maafisa watano wa kaunti ya Kilifi pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya Capital solutions kwa kujihusha na ufisadi.
Maafisa wa kaunti ya kilifi akiwemo Patience Umazi,John Mwangi , Sophie Mnyamai, Mohamed Silas Chuba , Julius Mwaidza pamoja na mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Capital Solutions Serah Musyimi wametiwa kwa kupitisha zabuni ya ununuzi wa mashua ya uokozi kwa shilingi milioni 14 na laki nane kinyume cha sheria.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari mkurugenzi wa tume ya EACC kanda ya Pwani Njeru Gishangi amesema sita hao walitekeleza ubadarifu wa fedha hizo mnamo mwaka wa 2016 hatua iliyopelekea maafisa wa EACC kuanzisha uchunguzi wa kina.
Maafisa hao ambao wamehojiwa kwa takriban masaa sita katika afisi za EACC huko Malindi wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi na wanatarijiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho.