Maafisa wawili wa polisi jamii katika eneo la Magogoni huko Kisauni Kaunti ya Mombasa wanauguza majeraha mabaya ya mapanga baada ya kuvamiwa na genge la Vijana alfajiri ya leo.
Afisa mkuu wa polisi wa eneo la Kisauni Julius Kiragu amesema wawili hao Vincent Simiyu na Said Omar walikuwa kwenye doria zao za kila siku ambapo wamekumbana na genge la zaidi ya Vijana 20 waliyojihami kwa mapanga na kuanza kuwakatakata.
Vijana hao vile vile wamevamia nyumba kadhaa katika eneo hilo la Mtopanga na kuwajeruhi wakaazi wengine alfajiri ya leo.
Simiyu yuko katika hali mahututi katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani, huku Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika likitaka polisi kulikabilii genge hilo la wahalifu.
Tayari Kiragu amesema uchunguzi unaendelezwa huku polisi wakiimarisha oparesheni dhidi ya genge hilo la majambazi.