Maafisa wakuu wa kitengo cha fedha, uhasibu na uagizaji katika Serikali ya kaunti ya Kwale wamehojiwa na kamati ya bunge la kaunti hiyo kuhusu fedha na uekezaji kutokana na sakata ya ubadhirifu wa fedha.
Maafisa hao ni pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha fedha Athman Mwatunza, pamoja na Abdallah Maningi na Wakili Zumo Kevin, wamefika mbele ya kamati hiyo ili kueleza matumizi ya fedha za mwaka wa 2017/2018 baada ya ripoti ya ubadharifu wa fedha kutolewa.
Akizingumza na Wanahabari baada ya kufanyika kwa kikao hicho, Mwenyekiti wa kamati hiyo Patrick Mangale amesema watatu hao walikosa kuzingatia sheria kuhusu matumizi ya fedha.
Mangale hata hivyo amesema maafisa hao walipeyana kandarasi kwa kampuni mmoja kufuatilia deni la shilingi milioni 46 zilizotolewa na serikali ya kaunti ya Kwale kwa wafanyibiashara kama mikopo.
Mwenyekiti huyo amesema maafisa hao walikiuka sheria ya kutoa zabuni sawia na kulipa shilingi milioni mbili kwa kampuni hiyo licha ya kampuni hiyo kukosa kutekeleza majukumu yake.
Wakati uo huo amedokza kuwa baada ya vikao hivyo kamati hiyo itaandaa ripoti na kuiwasilisha bungeni.