Story by Gabriel Mwaganjoni-
Maafisa wawili wa polisi wamejiuwa kwa kujipiga risasi katika visa tofauti katika kaunti ya Mombasa.
Kulingana na taarifa kutoka kwa wakuu wa usalama kaunti ya Mombasa, Afisa wa GSU Dennis Kamau amepatikana nyumbani kwake katika eneo la Nyali akiwa amefariki mapema hii leo.
Afisa huyo alikuwa katika kikosi maalum kinachotoa ulinzi kwa maafisa wa ngazi za juu Serikalini na anadaiwa kujipiga risasi kichwani na kufariki papo hapo.
Katika tukio la pili, Afisa wa polisi David Koech anayehudumu katika kituo cha polis cha Concordia eneo la Kiembeni kaunti ya Mombasa amejipiga risasi kifuani na kujiua papo hapo katika tukio tata.
Polisi wamepata bunduki aina ya AK-47 na jumla ya risasi 29 kwenye kasha la risasi ya bunduki hiyo.
Uchunguzi tayari umeidhinishwa huku miili hiyo miwili ikipelekwa katika makafani ya hospitali kuu ya rufaa kanda ya Pwani.