Idara ya usalama nchini, imetangaza kuwa maafisa wote wa polisi pamoja na wale wanaolenga kujiunga na kikosi cha polisi nchini, watalazimika kupokea mafunzo maalum kwa kipindi cha miezi sita kuhusu teknolojoia, habari na mawasiliano.
Akito tangazo hilo, wakati wa uzidunzi wa mfumo mpya wa mawasiliano na teknolojia maarufu IMS katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Kilifi, Waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matiangi amesema mfumo huo utaimarisha kikosi hicho na kuimarisha usalama.
Waziri Matiangi amesisitiza kuwa mfumo huo utasaidia pakubwa katika kuhakikisha matukio yote yanayoripotiwa katika idara ya polisi yanafuatiliwa na kutekelezwa kwa uwazi kupitia teknologia hiyo.
Waziri Matiangia alikuwa ameandamana na Waziri wa Teknoljia na mawasiliano nchini Joe Mucheru ambaye ameunga mkono kauli ya Waziri Matiangi pamoja na Inspekta jenerali wa Polisi nchini Joseph Boinet aliyewataka maafisa wa polisi kuhakikisha usalama na Amani unadumishwa kote nchini.
Taarifa na Charo Banda.