Picha kwa hisani –
Maafisa wa maabara wanaohudumu katika vituo vya afya vya umma nchini wameanza rasmi mgomo wao hii leo.
Akithibitisha mgomo huo katibu katika muungano wa maafisa wa maabara nchini Clifford Randa amesema maafisa hao wataendelea na mgomo hadi pale serikali,wizara ya afya na serikali za kaunti zote 47 watakaposikiliza mapendekezo yao.
Clifford amesema serikali kuu na zile za kaunti wameshindwa kutia saini mkataba wa makubaliano sawa na kutowapa maafisa wa maabara vifaa madhubuti vya kuwakinga na maambukizi ya virusi vya corona wanapokua kazini.
Hayo yakijiri wauguzi na madaktari katika kaunti ya Mombasa wameapa kuendelea na mgomo wao ulioanza rasmi mwaka uliopita,wakiilaumu serikali ya kaunti hio kwa kuwapa vitisho badala ya kuwatimizia mahitaji yao.