picha ya mmoja wa wahudumu
Wizara ya afya kaunti ya Kwale imelazimika kuwaagiza maafisa wa afya wa nyanjani waliokua mampumzikoni kurejea kazini ili waendeleze hamasa za nyumba hadi nyumba kuhusu ugonjwa wa Corona.
Waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya Kwale Francis Gwama amesema maafisa hao tayari wamepewa mafunzo ya kutosha kuhusiana na ugonjwa ambao visa vya maambukizi vinazidi kuongezeka nchini.
Gwama vile vile amewataka wakaazi wa kaunti hio ya Kwale kupiga ripoti kwa vitengo husika punde wanapohisi kuwa na dalili za maambukizi ya ugonjwa huo.