Picha kwa hisani –
Zaidi ya watu 60 wafa maji baada ya boti kuzama katika mto Congo. Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema watu 300 wameokolewa lakini inakisiwa kuwa watu wengine 200 hawajulikani walipo baada ya ajali hiyo.
Wakazi wanasema boti hio iligonga mwamba mashariki mwa mji mkuu wa Kinshasa, wakati walipokuwa wakisafiri usiku, huku safari za majini nyakati za usiku zikiwa zimepigwa marufuku nchini humo.
Waziri wa masuala ya kibinadamu,nchini humo Steve Mbikayi, ametaka wamiliki wa boti hio kushtakiwa.
Kuna barabara chache nchini DRC na shughuli nyingi za usafirishaji wa mizigo na abiria hufanywa kwa njia ya mto.