Picha kwa hisani –
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika limeimarisha uchunguzi wake kuhusu tukio la mauaji ya mwanamke mmoja katika eneo la Jilla, huko Bamba Kaunti ya Kilifi.
Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika hilo Mathias Hezron Shipetta, amesema mwanamke huyo kwa jina Neema George Karisa mwenye umri wa miaka 24 na mama wa mtoto mmoja aliuwawa kinyama kwa kukatwa shingo na mumewe.
Shipetta amesema wawili hao walikua katika mzozo wa nani atakayesalia na mtoto wao mdogo.
Shipetta amewataka Maafisa wa kituo cha polisi cha Bamba kuharakisha uchunguzi huo akisema juma zima sasa mumewe Neema ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji hayo Boni Odari hajatiwa nguvuni.
Shipetta japo amekiri kwamba kumeshuhudiwa visa vingi vya migogoro na dhuluma za kijinsia miongoni mwa wanandoa,amewataka wanandoa kutafuta ushauri kutoka kwa wadau wa maswala ya jinsia na Viongozi wa kidini.
Tayari mwili ma marehemu umefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Kilifi.