Story by Hussein Mdune
Mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale Mhandisi Lung’anzi Chai amemtangaza rasmi mgombea mwenza wake wa kinyang’anyiro cha ugavqna wa kwale wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Lung’azi amemtaja Kavwa Said Mwakaribu kuwa mgombea mwenza, akidai kwamba mwanamke huyo ana tajriba ya utendakazi kwani aliwahi kuhudumu kama Naibu mkufunzi mkuu wa taasisi ya mafunzo ya utabibu nchini KMTC tawi la Kwale na amechangia mengi hasa katika sekta ya Afya.
Akizungumza katika halfa hiyo iliyoandaliwa katika kijiji cha Golini eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale, Lung’anzi ametaka wanasiasa wapewe nafasi ya kuuza sera zao ili kuhakikisha kaunti ya Kwale inapata viongozi bora.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa Lung’azi Kavwa Said Mwakaribu
ameahidi kushirikiana na Lung’anzi ili kuhakikisha wakaazi wa kaunti ya Kwale wananufaika kimaendeleo.