Story by Hussein Mdune–
Mgombea wa kiti cha ugavana kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha PAA Lung’anzi Chai Mangale ameahidi kuboresha sekta ya kilimo kaunti ya Kwale endapo atanyakua kiti hicho.
Akiongea baada ya kupokea cheti chake kutoka kwa Tume ya IEBC katika ukumbi wa GTI eneo la Matuga kaunti ya Kwale, Lung’anzi amesema atahakikisha vijana wanapata ajira sawa na kuinua viwango vya utalii.
Kiongozi huyu amewataka wakaazi wa Kwale kudumisha amani wakati huu wa kampeni za uchaguzi huku akiwataka kutotumiwa vibaya na wanasiasa kwa misingi ya kikabila, dini na siasa.
Kwa upande wake Athuman Mwarora ambaye ni mgombea mwenza wake ameahidi kushirikiana na Lung’anzi ili kuzitatua na changamoto mbalimbali.