Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha PAA Lung’anzi Chai Mangale ameahidi kuboresha sekta ya elimu katika kaunti hiyo iwapo atachaguliwa kuwa gavana.
Lung’anzi amekashfu vikali hatua ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoneza uvumi kwamba fedha za basari katika kaunti hiyo zinatatolea kwa ubaguzi iwapo atakuwa gavana, akisema madai hayo hayana ukweli wowote kwani mikakati ya kufanikisha elimu bora itaidhinishwa.
Akizungumza katika eneo bunge la Matuga wakati wa mikutano yake ya kisiasa, Lung’anzi amewasihi wapinzani wake wa kisiasa kufanya kampeni zao kwa amani na wala sio kueneza uvumi ambao huenda ukachangia migawanyiko ya kijamii.
Wakati uo huo amewarai wakaazi wa kaunti ya Kwale kuwachagua viongozi wenye malengo ya kuchangia maendeleo mashinani huku akiwataka wakaazi kujitenga na saisa za vurugu.