Picha Kwa Hisani –
Muigizaji wa filamu za Bongo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amezungumza kuhusu swala la kuwapa uhuru watoto kutumia mitandao ya kijamii na kusema kuwa ataangalia umri wa mtoto wake na kumpa mipaka kwa sababu ni vitu ambavyo vina athari kubwa mtoto.
“Kiukweli hata mimi inshaallah nikijaaliwa watoto, watu watawaona shuleni, clinic au barabarani yaani sitawaficha ila watawaona kwenye maisha ya kawaida tu, kuna kipindi nilikuwa nafanya tofauti katika malezi ya mdogo wangu ila akili ikaja kubadilika baadae” – alisema Lulu.
Aidha, muigizaji huyo ameitaja mitandao kuwa chanzo kikuu cha kuleta madhara katika maisha ya watoto. Pia aliwashauri wazazi kutowatambulisha watoto mitandaoni hadi pale ambapo umri utaruhusu na kujichagulia maisha hayo wenyewe.
“Huku mitandaoni tupambane wenyewe tu, lakini kama mtoto atafika umri wa kuamua anataka nini ‘it’s okay’ wazazi ku-support ila kwa mipaka fulani maana sio kwamba mitandao ndio chanzo kikuu cha kuleta negative impact kwa mtoto, ila ni moja ya chanzo na kiko ‘very tricky’ ni kuomba Mungu pia” aliongeza Lulu.
Lulu amezungumzia swala hilo kufuatia stori zinazoendelea kwa sasa kuhusu msanii wa filamu Kajala Masanja na mtoto wake wa kike Paula Masanja maarufu mitandaoni kama Paula Kajala.