Picha kwa Hisani –
Chama cha mawakili nchini LSK kimewasilisha kesi Mahakamani, kikipinga masharti yaliotangazwa hivi majuzi na baraza la kitaifa ya ushauri wa kiusalama nchini dhidi ya usalama wa taifa.
Chama kinachoonzwa na Rais wake Nelson Havi imetuma baadhi ya Mawakili Mahakamani wakiitaka Mahakama kumzuilia kumzuia Inspekta mkuu wa Polisi nchini Hillary Mutyambai pamoja na maafisa wake kutoingilia mikutano ya umma.
LSK pia inapinga masharti hayo ikisema yanahujumu haki za wakenya kwani Katiba ya nchi imeweka wazi kuhusu jinsi wakenya wanavyofaa kuandaa mikutano ya umma.
Masharti hayo ambayo LSK inayapinga ni pamoja na agizo lililotolewa na Baraza la kitaifa la ushauri wa kiusalama kuwa viongozi wanaopanga kuandaa mikutano ya umma ni lazima wamjulishe Kamanda wa polisi wa eneo husika kwa kipindi cha siku 3 hadi 14 kabla ya kuandaa mikutano hiyo.