Picha Kwa Hisani.
Sehemu ya Wakenya wenye hamaki wametumia mitandao ya kijamii kupinga bei ghali ya bidhaa muhimu haswa bidhaa za chakula.
Wananchi hao wamezindua Kampeni Mitandaoni wakiitaka serikali ipunguze bei ya Chakula.
es
Hivi karibuni, wanamitandao kutoka humu nchini wamelazimika kujifinya zaidi ili kumudu bei ya vyakula. Kupitia alama ya reli #lowerfoodprices, iliyokuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii, huku wakiomba serikali kuingilia kati na kupunguza bei ya vyakula.
Pia, waliwataka wagombea wa nyadhifa mbalimbali za kisiasa kuweka mbele masilahi yao wakisema hawataweza kupiga kura wakiwa na njaa kabla ya Agosti 9.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii walihoji kuwa kwa sasa, Wakenya wengi hawana uwezo wa kula milo mitatu kwa siku.