Picha kwa hisani –
Ofisi ya Rais imetangaza kuwa kuanzia tarehe 22 mwezi huu, Mawaziri wote watakwenda kwa mapumziko katika kipindi cha majuma mawili.
Mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinywa amesema mazungumzo ya rais na idara mbalimbali pamoja na wageni watakaozuru nchini yataendelea bila ya kupingwa licha ya kuwa atakuwa na shuhuli tofauti za kibinafsi.
Kinywa ameweka wazi kuwa kalenda na taratibu za baraza la kitaifa la usalama nchini, zitaendelea jinsi zilivyopangwa ili kuhakikisha usalama wa taifa unalindwa hasa wakati huu wa shamrashamra za sherehe za Krismasi na mwaka mpya.
Wakati uo huo amedokeza kuwa huduma zote za serikali zitaendelea kutolewa kwa ufanisi huku amesema kalenda ya baraza la mawaziri ya mwaka wa 2021 itazingatia juhudi za kudhibiti kabisa ugonjwa wa Covid-19.