Story by Hussein Mdune-
Huenda tabia wa wanawake kutumiwa vibaya wakati wa kampeni za uchaguzi ikakomeshwa iwapo wanawake wenyewe watatambua uongozi wa Mwanamke.
Haya ni kulingana na mgombea wa kiti cha ubunge wa Kinango kwa tiketi ya chama cha Wiper Neema Kwekwe Chiwai.
Kwekwe amesema wanawake wako na uwezo wa kuboresha maendeleo mashinani iwapo watapewa nafasi na malengi hayo yatatimia iwapo wanawake waungana.
Mwanasiasa huyo ameahidi kuwawezesha wanawake katika biashara sawa na vikundi mbalimbali vya maendeleo iwapo atapewa nafasi hiyo ya ubunge.
Hata hivyo amewataka wanawake katika eneo bunge hilo kujitenga na wanasiasa wasio na ajenda za maendeleo.