Taarifa na Hussein Mdune.
Shirika linaloangazia masuala ya elimu kaunti ya Kwale (KWEA) limewataka wazazi kaunti hio kufatilia miendendo ya watoto wao msimu huu wa likizo ya mwezi agost ili wasijihusishe na uhalifu na ngono za mapema.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bi Sabina Saiti amesema msimu wa likizo vijana hujiunga na marafiki wabaya hali inayowasukuma kujiingiza katika makundi yasiofaa.
Hata hivyo amesema kuwa mara nyingi watoto wa kike upata ujauzito kutokana na hatua ya wazazi kuzembea katika kutekeleza majukumu yao ya ulezi.