Taarifa na Amina Fakii
Usimamizi wa kampuni ya usambazaji maji kaunti ya Kwale (KWASCO), imeweka wazi kuwa imekatiwa umeme kufuatia malimbikizi ya madeni inayodaiwa na kampuni ya Kenya Power.
Mwenyekiti wa bodi inayosimamia kampuni hiyo ya maji Francis Nzai amesema tangu mwezi wa Januari mwaka huu, kampuni hiyo inawadai wateja wake takraban shilingi milioni 14, hali ambayo imepelekea kushindwa kulipa madeni yake.
Hata hivyo Nzai amesema ili kuafikia malengo ya kampuni hiyo ya kutoa huduma bora za maji, ni lazima ikusanye fedha zaidi ya shilingi milioni 13 kila mwezi lakini kwa sasa kampuni hiyo inakusanya shilingi milioni 7 hadi 8 kutoka kwa wateja wake.