Picha kwa hisani –
Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale inachunguza kisa ambapo mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 12 katika eneo la Matuga amepachikwa uja uzito katika mazingira tatanishi.
Naibu kamishana katika eneo la Matuga Alexander Mativo amesema wamegundua kuhusu kisa hicho wakati wa msako wa nyumba hadi nyumba wa wanafunzi ambao hawajarejea shule unaoendelezwa na maafisa tawala.
Mativo amesema mwanamume aliyetekeleza unyama huo ameingia mafichoni na kwamba maafisa wa polisi wameidhinisha msako mkali dhidi yake ili kuhakikisha anatiwa nguvuni na kufunguliwa mashtaka.
Mativo amekiri kuwepo na ongezeko la dhulma za kingono zinazotekelezwa na watu wa karibu wa waathiriwa .
Hata hivyo mbunge wa matuga Kassim Tandaza amelaani kitendo hicho akishikilia kwamba wanaotekeleza dhulma za kingono lazima wahasiwe.