Kifo cha msanii Amiri Athuman maarufu kama Mzee Majuto kimewaacha wengi na majonzi yasiyokuwa na kipimo.
Mauti yake yamechoma mioyo ya wengi wakubwa kwa wadogo, tajiri na maskini kwani chanzo cha kicheko chao kila wanapotizama runinga hakipo tena.
Licha ya mengi kusemwa kuhusu mkongwe huyu katika tasnia ya uigizaji alipenda sana kuzuru Kenya mara kwa mara. Taifa la Kenya aliliona kama nyumbani.
Katika mahojiano yake ya mwisho na kituo cha Radio Kaya, Majuto alifichua sababu ya kuipenda Kenya.
Kulinagana naye Kenya ndiyo iliyokuwa chimbuko lake. Mzee Majuto alipata mafunzo ya uigizaji kutoka kwa Bakari Suleiman Mwamgula mwana sanaa maarufu kutoka eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa. Mzee Majuto alikiri kuwa mafunzo ya Mwamgula ndiyo yaliyomsaidia pakubwa katika tansia ya uigizaji.
Majuto alizaliwa mwaka wa 1948 na kuanza uigizaji akiwa na umri wa miaka tisa mwaka wa 1958.
Taarifa na Dominick Mwambui.