Afisa wa maswala ya watoto gatuzi dogo la Nyali Emannuel Tendet amesema kutokana na kuongezeka kwa visa vya kuvunjika kwa ndoa mjini Mombasa kumekuwa na ongezeka la visa vya dhulma kwa watoto.
Akiongea mjini Mombasa afisa huyo amesema kuwa watoto wengi mjini Mombasa wanaishi kwenye malezi ya mzazi mmoja hatua inayopelekea wengi wao kujiunga na uhalifu.
Hata hivyo amesema kuwa malezi ya mzazi mmoja hayawezi kukidhi mahitaji ya mtoto hivyo basi akawahimiza wazazi kujitenga na tabia za talaka za mara kwa mara ilikuona kwamba watoto wanapata malezi bora.
Taarifa na Hussein Mdune.