Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wakenya kuchukua hatua ya kusameheana na kushirikiana, akisema hiyo ndio njia pekee ya taifa hili kupiga hatua kimaendeleo, amani na umoja.
Akizungumza katika ikulu ya Nairobi wakati wa maombi ya kitaifa aliyoandaliwa siku ya Jumamosi Oktoba 10, Kiongozi wa nchi amesema ushirikiano huo utawezesha taifa hili kupiga hatua katika kupambana na janga la Corona.
Rais Kenyatta amewasihi pia wakenya kuzidi kuliombea taifa huku akiwapongeza wahudumu wa afya, viongozi wa idara ya serikali na viongozi wengine nchini kwa kuonyesha ushirikiano wakati huu ambapo taifa linakabiliwa na janga la Corona.
Naye Askofu mkuu wa Kanisa la kianglikana nchini Jackson Ole Sapit na mwenzake Askofu David Kamau kwa pamoja wamesema ni kupitia maombi ndipo taifa litakua huru.