Story by Ngumbao Jeff-
Bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama cha UDA imesema itaandaa mazungumzo ya kina kuhusu swala la kura za mchujo za chama hicho iwapo zitafanyika kwa kutumia sajili ya chama hicho au sajili ya Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Wanachama wa bodi hiyo wakiwemo Salome Beacco na Raphael Chimera wamesema swala hilo litajadiliwa kwa kina ili kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika kura hizo za mchujo.
Viongozi hao wameweka wazi kwamba uamuzi huo utasaidia pakubwa kuhakikisha zoezi hilo la kura za mchujo zinafanyika kwa njia huru na haki kote nchini.
Kwa upande wake mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kilifi kupitia chama cha UDA Aisha Jumwa amesema tayari wanachama wa chama hicho wamekubaliana kwa kauli moja kutumia sajili ya Tume ya IEBC katika kura hizo za mchujo.