Picha kwa hisani –
Chama cha waalimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPET kimeitaka serikali kufungua shule za humu nchini kwa awamu kwa kuwapa watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne kipaumbele.
Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi Mwenyekiti wa chama hicho Amboko Milemba amesema punde shule zitakapofunguliwa wizara ya fedha pia inapaswa kutuma mgao wa fedha kwa shule zote za umma nchini ilikuwezesha shule hizo kuwa na fedha za kujimudu.
Milemba vile vile ameitaka wizara ya elimu kufanya utathmini kubaini idadi kamili ya shule za kibinafsi ambazo zimefungwa kufikia sasa kwa kukosa fedha za kujimudu kipindi hiki cha corona,na wanafunzi wa shule hizo wasajiliwe katika shule za umma.
Wakati uo huo mwenyekiti huyo wa KUPPET ameitaka serikali kuhakikisha wanafunzi wote milioni 12 wa shule za msingi na kibinafsi nchini wanapewa barakoa wanapokua shuleni ili kuzuia maambukizi ya corona.