Picha cha hisani –
Vyama vya waalimu nchini KNUT na KUPPET vimetitishia kuwaondoa waalimu wanaohudumu katika maeneo ya Kapedo,kaunti ya turkana na Baringo kufuatia utovu wa usalama unaoshuhudiwa katika maeneo hayo.
Katika taarifa ya pamoja iliotumwa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa KUPPET Omboko Milemba, amesema wametoa makataa ya siku saba kwa serikali kurejesha hali ya utulivu katika maeneo hayo.
Kwa upande wake katibu wa chama cha KNUT Tawi la Baringo Joshua Cheptarus amewataka waalimu wanaohudumu katika kaunti hio kusitisha majukumu yao na kuondoka eneo hilo mara moja iwapo watahisi maisha yao yako hatarini.
Haya yanajiri huku takriban watu kumi wakiaga dunia mamia wakihama makaazi yao kufuatia mzozo unaoushudiwa kati ya polisi na majangili katika eneo la Kapedo kwenye mpaka wa kaunti za Turkana na Baringo kwa takriban majuma mawili sasa.