Idara ya usalama katika kaunti ya Mombasa imeanzisha mpango wa kurahisha huduma ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa kaunti hiyo.
Kamishna wa kaunti hiyo Evans Achoki amesema kuwa mpango huo utaendelezwa kwa siku thelathini, akiwasihi wazazi kujitokeza kwa wingi kuhakikisha watoto wao wanapata vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi bila malipo.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa baada ya kuzindua rasmi mpango huo Achoki amesema kuwa wameshirikana na machifu wa kaunti hiyo kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji vyeti vya kuzaliwa inaboreshwa zaidi.
Wakaazi katika kaunti hiyo hata hivyo wameeleza furaha yao kuhusu mpango huo wakisema umewarahisishia kupata cheti hicho muhimu cha watoto wao.