Picha kwa hisani –
Gavana wa Kilifi Amason Jeffa Kingi ametaja kupasuka kwa mabomba ya kusambaza maji katika kaunti hio kama miongoni mwa changamoto zinazosababisha uhaba wa mara kwa mara wa maji katika kaunti hio.
Akizungumza na wanahabari Kingi amekiri kuwepo na uhaba wa maji ndani ya kaunti hio,akisema tatizo hilo limeshughulikiwa na idara husika na kwamba huduma za maji ndani ya kaunti hio zitaimarika.
Kingi amesema deni la umeme ambalo kampuni ya maji ya kaunti hio inadaiwa na kampuni ya usambazaji umeme nchini tayari limelipwa na shughuli ya kusambaza maji imeanza rasmi katika kituo kikuu cha maji cha baricho.