Story by Our Correspondents-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Msambweni kwa tiketi ya chama cha Wiper Swalha Hemed Sarai ameahidi kushinikiza mgao wa fedha za basari kuongezwa sawa na kuidhinishwa kwa hoja bungeni itakayochangia mgao huo kufikia kiwango cha kuwawezesha wazazi kumudu gharama ya masomo.
Katika mahojiano ya kipekee kwenye kituo cha Radio Kaya katika kipendi ya Voroni Enehu, Swalha amesema hatua hiyo itachangia wazazi kupata kiwango cha juu cha fedha hizo kwa watoto wao kutoka shilingi elfu tano hadi shilingi elfu 20.
Swalha amesema kuna haja ya mikakati mwafaka kuidhinishwa iwapo viongozi wana malengo ya kuwasaidia wanafunzi kufanya vyema shuleni huku akiahidi kuhakikisha anawekeza zaidi katika swala la elimu iwapo atachaguliwa.
Wakati uo huo ameahidi kuhakikisha walimu wa dini wanajumuishwa katika swala la mishahara, akisema walimu wa madrassa na wale wa dini ya kikristo wamekuwa wakitoa mafunzo ya dini kwa watoto bila ya kulipwa mshahara.