Story by Our Correspondents-
Kenya inajiungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya bahari dunia ikiwa lengo kuu ni kuhamasisha binadamu kuhusu manufaa ya bahari.
Shirika la umoja wa mataifa UN limehimiza mataifa kuweka sheria thabiti ambazo zitalinda Bahari kutokana na uharibifu ambao mara nyingi umeonekana kuchangiwa na binadamu.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema ni wakati sasa wa ulimwengu kutambua kwamba ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu na malengo ya mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kunahitaji hatua za haraka ili kudhibiti uchafuzi wa bahari.
Guterres amesema japo bahari inazunguka asilimia 70 ya ardhi, kuna haja ya mataifa wanachama kuchukua jukumu la kulinda viumbe vya habari ili kuwezesha watu zaidi ya milioni 40 kunufaika na raslimali za bahari ifikapo mwaka 2030.
Hata hivyo kauli mbiu ya mwaka huu ni kuihuisha, hatua ya pamoja ya habari.