Story by Ali Chete –
Mwenyekiti wa chama cha kitalii Pwani KCTA Victor Shitaka, amesema sekta ya utalii imeimarika kufuatia hatua ya serikali ya kulegeza masharti dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Shitaka amesema watalii wa ndani kwa ndani pamoja na wale wa mataifa ya kigeni wamekuwa na ujasiri wa kuzuru maeneo tofauti ya kitalii katika eneo la Pwani baada ya masharti hayo kulegezwa na serikali.
Hata hivyo, ameahidi kwamba wataendelea kuzingatia masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona ikiwemo kuosha mikono.