Kufungwa kwa baadhi ya kampuni za mawakala wa forodha jijini Mombasa kumepelekea vijana wengi waliokuwa wameajiriwa kwenye kampuni hizo kurandaranda mitaani na kuwa tishio kwa usalama.
Shirika la kutetea haki za kibanadamu la HAKI AFRIKA limedai kuwa hali hii imechangia vijana kujiunga na magenge ya kihalifu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Khalid Hussein amesema kuwa vijana wengi baada ya kuachishwa kazi kwenye kampuni hizo wameanza kuihangaisha jamii mitaani.
Khalid ameitaka serikali ya kaunti y Mombasa na ile kuu kupitia idara ya usalama kushirikiana ili kukabiliana na visa vya uhalifu na mauaji ya kiholela katika kaunti ya Mombasa.
Taarifa na Hussein Mdune.